1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Gates na Bush wazungumzia Iraq.

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgV

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amezungumza na rais George W. Bush huko Camp david katika jimbo la Marekani la Maryland.

Mazungumzo hayo yalilenga katika ziara ya waziri huyo wa ulinzi nchini Iraq hivi karibuni.

Bush anatarajiwa kuijadili Iraq na kundi la maafisa wa usalama wa taifa wiki ijayo.

Msemaji wa Bush amesema kuwa rais amefurahishwa na hatua za maendeleo zinazochukuliwa ili kubadili sera za Marekani kuelekea Iraq.