1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Gharama za vita zitalipwa hatua kwa hatua

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3K

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kutoa pesa kwa mikupuo,kugharimia vita vya Iraq.Kura 221 zimeunga mkono uamuzi huo na 205 zimepinga.Hatua hiyo kwa mara nyingine tena inakwenda kinyume na Rais George W.Bush ambae ametishia kutumia kura ya turufu kupinga uamuzi wa aina hiyo.Baraza la Wawakilishi limeidhinisha kutoa Dola bilioni 43,lakini linataka kuona maendeleo ya kuleta utulivu nchini Iraq ifikapo mwezi Julai,kabla ya wabunge kutoa kifungu cha pili cha pesa zipatazo Dola bilioni 53.Juma lililopita,Rais Bush alitumia kura ya turufu kupinga mswada uliotaka kufungamanisha malipo ya kugharimia vita na ratiba ya kuviondosha vikosi vya Kimarekani kutoka Irak.Spika wa bunge,Nancy Pelosi wa chama cha Kidemokratik amesema,kura iliyopigwa siku ya Alkhamisi,imekomesha kile alichokiita “hundi iliyo wazi kwa vita vya rais”.