1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: India kupatiwa nishati na teknolojia ya nyuklia

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl6

Bunge la wawakilishi nchini Marekani,limepitisha mswada wa sheria ya kihistoria kuruhusu kuipatia India nishati na teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya umma.Wabunge,kwa uwingi mkubwa walipiga kura kuunga mkono mswada wa sheria hiyo.Sasa,mswada huo unahitaji kuidhinishwa na Seneti,kabla ya rais George W.Bush kutia saini yake na kuwa sheria.Kuambatana na makubaliano hayo ya utata,India iliyotia saini mkataba wa kuzuia ueneaji wa silaha za nyuklia kwa ufupi NPT,itapatiwa teknolojia na nishati ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia na badala yake India iruhusu ukaguzi wa vinu vyake vya nyuklia.Lakini wakosoaji wanasema,kwa sababu ya makubaliano hayo,itakuwa vigumu zaidi kuweka sheria dhidi ya madola yenye miradi ya nyuklia,kama vile Korea ya Kaskazini na Iran;vile vile ni mfano wa hatari kwa madola mengine yanayotaka kuwa na miradi ya nyuklia.