1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Iran itengwe ikiwa haitositisha mradi wake wa kinuklia

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsz

Rais George W.Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert wametoa mwito kwa Syria na Iran kubadilisha miilekeo yao.Wakati huo huo viongozi hao katika mkutano wa mjini Washington wamepinga kwa hivi sasa kuwa na majadiliano ya moja kwa moja pamoja na nchi hizo mbili.Bush amesema,hatua zichukuliwe ikiwa serikali ya Teheran haitotekeleza madai ya magharibi kuhusu mradi wake wa kinuklia.Akaongezea kuwa hatua nzuri ya kwanza ni kushirikiana pamoja kuchukua hatua ya kuitenga Iran.Olmert amesema kuwa anaunga mkono juhudi zinazoongozwa na Marekani kutaka kuiwekea Iran vikwazo kwa sababu ya kukataa kusitisha mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.Lakini amesisitiza kuwa Israel haitafuti mpambano na Teheran.