1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Jeshi lakaripia wanaanga 70.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dz

Jeshi la anga nchini Marekani limewakaripia wanaanga 70 wa jeshi hilo waliohusika katika ajali ya ndege ya kijeshi yenye silaha za kinuklia chapa B-52 ya mashambulizi. Uchunguzi umegundua uzembe mkubwa kuhusiana na kupuuzwa kwa sheria.

Wakati wa kurusha ndege hiyo kutoka Minot karibu na mpaka na Canada kwenda Barksdale katika jimbo la Louisiana , ndege hiyo ya kivita B-52 ilikuwa na makombora sita ya kinuklia. Mwanzoni hakuna mtu aliyetambua makosa hayo. Makombora hayo yalikuwa yanapelekwa Louisiana , lakini silaha hizo za kinuklia zilibidi kuondolewa mapema.