1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Juhudi za kufufua majadiliano ya amani zaungwa mkono

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVY

Wapatanishi wa pande nne kuhusika na mgogoro wa Mashariki ya Kati,wanaokutana mjini Washington wameunga mkono juhudi za Marekani kutaka kufufua majadiliano ya amani kati ya Israel na Wapalestina.Kundi hilo la pande nne ambalo hujumuisha Umoja wa Ulaya,Marekani,Umoja wa Mataifa na Urussi,limeeleza wasi wasi wake kuhusu mapambano yalioshika kasi hivi karibuni kati ya makundi hasimu ya Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.Kundi hilo pia limesisitiza msimamo wake kuhusu vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa mwaka mmoja wa nyuma dhidi ya serikali ya Kipalestina inayoongozwa na Hamas.Kundi hilo linataka chama cha Hamas kitangaze kuacha kutumia nguvu,kitambue haki ya kuwepo taifa la Israel na vile vile kiheshimu mapatano yaliokuwepo kati ya Mamlaka ya Wapalestina na Israel.