1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ziarani Marekani

5 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdE

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameshauriana na Rais wa Marekani George Bush kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya bara la Ulaya na Amerika.

Hiyo ndiyo ziara ya kwanza ya Bibi Merkel katika nchi ya kigeni tangu Ujerumani ilipokamata urais wa Umoja wa Ulaya na uongozi wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda G8.

Rais Bush alimpongeza Merkel kwa wito wake wa kuanzisha harakati mpya ili kutatua mzozo kati ya Wapalestina na Waisrail.

Kansela Angela Merkel alizungumzia umuhimu wa kulitilia maanani suala hilo la Mashariki ya Kati na kusema:

"Ninaamini kwamba Umoja wa Ulaya ukiwa miongoni mwa pande nne zinazoshughulikia mzozo wa Mashariki ya Kati, unaweza kutoa mchango muhimu kusaidia kutatua matatizo ya Mashariki ya Kati. Bila shaka hapa tuna jukumu kubwa la kutekeleza"

Rais George Bush amewaambia waandishi wa habari kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Condoleeza Rice, atazuru Mashariki ya Kati hivi karibuni na kisha kuwaarifu viongozi hao wawili kuhusu hali ilivyo.

Masuala mengine yaliyoshughulikiwa kwenye mashauriano hayo ni mzozo wa Iraq, Afghanistan, mradi wa Iran wa nishati ya kinyuklia pamoja na mzozo katika eneo la Darfur nchini Sudan.