1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Korea ya kaskazini yapata msaada kutoka Marekani.

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLq

Rais wa Marekani George W. Bush ameidhinisha msaada wa dollar milioni 25 kwa ajili ya nishati kwa Korea ya kaskazini ikiwa ni sehemu ya makubaliano ili utawala huo wa Pyongyang uachane na shughuli zake za kinuklia.

Korea ya kaskazini imekubali katika mwezi wa Februari kuachana na mpango wake wa kinuklia ili kuweza kupata msaada wa nishati kutoka Marekani na mataifa mengine.

Tangazo hilo limekuja wakati maafisa kutoka katika mazungumzo ya nchi sita , China, Japan, Russia, Marekani na Korea zote mbili, wakikutana mjini Beijing ili kufanyiakazi utekelezaji wa makubaliano hayo.

Marekani inataka kuhakikisha kuwa kinu cha kinuklia katika eneo la Yongbyon kinafungwa kabisa, na kuutaka utawala wa Korea ya kaskazini kuondoa wasi wasi kuwa unarutubisha madini ya Uranium.