1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Majeshi ya Marekani yatabakia Irak

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPe

Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Robert Gates amesema,upo uwezekano wa kupunguza idadi ya wanajeshi wa Kimarekani nchini Irak na kubakisha hadi 100,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2008.Lakini akaongezea,uamuzi wo wote wa kuondosha majeshi kutoka Irak,utategemea ile hali inayokutikana nchini humo.Hapo awali,Rais wa Marekani,George W.Bush aliarifu kuwa hadi katikati ya mwaka 2008,zaidi ya wanajeshi 20,000 wataondoshwa Irak. Akaeleza waziwazi kuwa majeshi ya Marekani yatakuwepo Irak,yeye atakapomaliza awamu yake miezi 16 ijayo.Hivi sasa,Marekani ina kiasi ya wanajeshi 168,000 nchini Irak.