1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani aionya Iran

22 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Df

Makamo wa rais wa Marekani Dick Cheney ameonya kwamba serikali ya Marekani haitokubali kuvumilia kuwepo kwa mipango ya kutengeneza silaha za nuklea ya Iran.

Akizungumza kwenye kikao cha sera ya Mashariki ya Kati Cheney ameielezea Iran kuwa ni kikwazo cha amani.Pia amerudia tena madai ya Marekani kwamba Iran inawaunga mkono waasi nchini Iraq.

Kauli hiyo ya Cheney inakuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais George W. Bush kuonya kwamba taifa lenye uwezo wa silaha za nuklea lran linaweza kupelekea kuzuka kwa Vita Vikuu vya Tatu Duniani.

Serikali ya Iran imekuwa ikisema kwamba mpango wake huo wa nuklea ni kwa ajili ya dhamira za amani tu.