1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani inafikiria upya mkakati wake kuhusu Irak

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtD

Serikali ya Marekani inataka kuchunguza mkakati wake kuhusu Irak,huku machafuko yakiendelea nchini humo.Siku ya Jumatatu rais George W.Bush atakutana na kamati huru itakyoongozwa na waziri wa kigeni wa zamani James Baker.Mkutano huo wa wajumbe wa Republikan na Demokrat utahudhuriwa pia na waziri wa mambo ya kigeni Condoleezza Rice,makamu wa rais Dick Cheney na balozi wa Marekani nchini Irak,Zalmay Khalilzad.Kiongozi wa majeshi ya Marekani,Jemadari-Mkuu Peter Pace amesema,kamanda wa vikosi vya Marekani nchini Irak,Jemadari George Casey,atashiriki katika majadiliano ya kushauriana juu ya mabadiliko ya mkakati.Kwa upande mwingine,wanasiasa mashuhuri wa Demokrat wamezungumzia juu ya mpango wa kuanza kurejesha nyumbani vikosi vya Marekani kutoka Irak,katika muda wa miezi minne hadi sita ijayo.