1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani ipunguze mashambulizi ya angani

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cf

Rais wa Afghanistan,Hamid Karzai ametoa mwito kwa Marekani kupunguza idadi ya mashambulizi yake ya angani dhidi ya wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan.Amesema,raia wengi wasio na hatia wameuawa katika mashambulizi ya aina hiyo.Rais Karzai,katika mahojiano yake kwenye televisheni ya Marekani CBS,akaongezea kuwa wananchi wa Afghanistan hawaelewi kwanini bado kuna haja ya kufanywa mashambulizi ya angani,miaka mingi baada ya nchi hiyo kuingiliwa kijeshi.Amesema,bila ya shaka kuna njia zingine za kupambana na wanamgambo hao.