1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani kuondoa majeshi yake Iraq?

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkW

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa maafisa wa Ikulu ya Marekani wanajadili iwapo rais George W. Bush anapaswa haraka iwezekanavyo kuanza kuyaondoa majeshi ya Marekani kutoka katika miji ya Iraq.

Gazeti hilo la kila siku limeelezea kuporomoka kwa uungaji mkono wa wajumbe wa baraza la Seneti kutoka katika chama cha Republican kuhusiana na mkakati wa rais kuielekea Iraq kuwa ni sababu ya uwezekano wa kutangazwa kwa hatua hiyo.

Katika ishara ya kuongezeka kwa wasi wasi katika utawala wa nchi hiyo, waziri wa ulinzi Robert Gates amefuta mipango ya ziara yake ya mataifa ya Latin Amerika wiki hii ili kuweza kuhudhuria mikutano juu ya Iraq.Gazeti la Washington Post wakati huo huo limesema kuwa ripoti ya kipindi cha mpito inayotarajiwa kutolewa wiki ijayo itafichua kuwa serikali ya waziri mkuu Nuri al-Maliki haijafikia malengo hadi sasa yaliyowekwa na Bush wakati alipotangaza mabadiliko ya sera zake, ikiwa ni pamoja na uongezwaji wa wanajeshi wa Marekani mwezi wa Januari mwaka huu