1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani kutoa msaada wa fedha kuimarisha vikosi vya rais Abbas

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAp

Marekani itatoa kiwango cha dola kiasi ya milioni 60 kama msaada wa kuimarisha vikosi vya rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas. Uamuzi huo umefikiwa baada ya wabunge wa Congress kuacha kupinga mpango huo.

Dola milioni 43 zitatumiwa kwa mafunzo na ununuzi wa vifaa kwa kikosi kinachomlinda rais Abbas.

Kiwango kingine cha fedha hizo kitatumiwa kuboresha usalama na miundombinu katika kituo cha kupitishia mizigo kati ya Israel na Ukanda wa Gaza.

Kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kupitia juhudi za waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, rais Mahmoud Abbas amesema atakutana na waziri mkuu wa Isreal, Ehud Olmert Jumapili ijayo. Hata hivyo rais Abbas hakutaja ni wapi mkutano huo utakakofanyika.

Mkutano huo utakuwa wa kwanza kati ya viongozi hao tangu walipokubaliana mwezi uliopita kukutana mara moja baada ya kila majuma mawili.