1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yailalamikia China.

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVe

Marekani imewasilisha malalamishi dhidi ya China kwenye Shirika la Biashara la Dunia, WTO, kwamba serikali hiyo inatoa ruzuku kwa kampuni zake.

Marekani inadai serikali ya China inazisadia kwa hali na mali kampuni zake kukabiliana kibiashara na kampuni za Marekani na mataifa mengine ya kigeni.

Wawakilishi wa kibiashara wanatarajiwa kushauriana kwa muda wa miezi miwili kutokana na hatua hiyo ya Marekani ili kupata ufumbuzi mwafaka.

Iwapo wahusika watashindwa kukubaliana, jopo la Shirika la Biashara la Dunia linatarajiwa kukutana kusuluhisha mzozo huo.