1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yakaribisha msaada wa kimataifa

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkq

Serikali ya Marekani imetoa mwito kwa jumuiya kimataifa kutoa mchango zaidi kutenzua mgogoro wa Irak.Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice,baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alisema,Marekani itakaribisha mchango wa mataifa mengine.Wakati wa ziara yake fupi mjini Washington,waziri Steinmeier aliashiria kuwa Ujerumani,kimsingi ipo tayari kusaidia kidplomasia katika Mashariki ya Kati.Wakati huo huo lakini alionya dhidi ya kuwa na matazamio makubwa.Amesema,Ujerumani haitochukua dhima ya kuwa mpatanishi.Akaongezea kuwa hata vikosi vya Kijerumani kama ilivyo hivi sasa,havitopelekwa Irak.Steinmeier amesharejea Berlin na amesema ameridhika na ziara yake.Akaongezea kuwa Marekani imetambua umuhimu wa bara la Ulaya.