1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yaungwa mkono kuhusu Mashariki ya Kati.

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVc
Rais Faure Gnassingbe wa Togo
Rais Faure Gnassingbe wa TogoPicha: dpa

Kundi la pande nne linaloshughulikia mzozo wa Mashariki ya Kati linalokutana mjini Washington, limeunga mkono harakati za Marekani za kutaka kufufua mashauriano ya amani kati ya Israil na Wapalestina.

Kundi hilo linalojumuisha Umoja wa Ulaya, Marekani, Umoja wa Mataifa na Russia limeelezea kufadhaishwa na ghasia zinazoendelea kati ya makundi ya Kipalestina kwenye ukanda wa Gaza.

Kundi hilo lilielekea kuunga mkono vikwazo vya kimataifa vya tangu mwaka mmoja vilivyowekewa serikali ya chama cha Hamas ili kikomeshe utumizi wa nguvu, na kuitambua Israil na pia kuheshimu mikataba yote iliyotiwa saini kati ya Mamlaka ya Wapalestina na Israil.