1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Msaada kupunguza mzigo wa madeni

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTq

Rais wa Marekani,George W.Bush ametangaza mradi wa kusaidia wamilikinyumba binafsi wapatao maelfu kadhaa,ambao wanakabiliwa na kitisho cha kufilisika.Wakati huo huo amesema,azma ya serikali si kusaidia watu walioamua kununua nyumba licha ya kujua kuwa hawana uwezo wa kulipa.Vile vile kutakuwepo sheria kali zaidi kudhibiti riba iliyopindukia kiasi.

Mzozo wa fedha uliozuka nchini Marekani, umesababishwa na mikopo iliyokuwa ikitolewa na benki kwa wateja wasio na uwezo wa kutosha wa kulipa madeni.Mzozo huo,umeathiri pia benki za kigeni-mojawapo ni benki ya Kijerumani ya Sachsen LB.