1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Msaada wa Dola milioni 1 kwa Darfur

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3P

Taasisi inayoongozwa na wacheza michezo ya sinema,Angelina Jolie na Brad Pitt imetoa mchango wa Dola milioni moja.Pesa hizo zitagharimia misaada ya kiutu katika jimbo la mgogoro la Darfur,magharibi mwa Sudan na nchi jirani Chad ambako mamia ya wakazi wa Darfur wanaishi kambini au hawana hata mahala pa kuishi.Angelina Jolie ni balozi wa ukarimu wa Halmashauri ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa UNHCR.Ofisi ya halmshauri hiyo mjini Washington imesema,mashirika matatu ya misaada ya kiutu,katika jimbo la Darfur, yanahudumia zaidi ya watu milioni 2 waliopoteza makazi yao.Na mashariki mwa Chad,misaada inatolewa pia kwa wakimbizi wengine 240,000.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa tangu kuanza kwa mapambano ya Darfur hapo mwaka 2003,si chini ya watu 200,000 wamepoteza maisha yao na wengine milioni 2.5 wamefukuzwa makwao.