1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwanadiplomasia aomba radhi kwa kuikosoa serikali ya Marekani juu ya Irak

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD02

Mwanadiplomasia moja wa Marekani ameomba radhi kutokana na matamshi yake kwamba sera za Marekani nchini Iraq zinaonyesha kiburi na ujinga. Siku moja baada ya matamshi yake kurushwa katika mahojiano na televisheni ya kiarabu ya Al-Jazeera, Alberto Fernandez aliandika barua ya kuomba radhi kupitia idara ya habari ya wizara ya mambo ya kigeni kwamba aliteleza ulimi. Hata hivyo, utawala wa rais Bush umekuwa ukikabiliwa na shinikizo kali ili ufikirikie mikakati mipya juu ya Irak baada ya mkutano na makamanda wakuu wa kijeshi. Wanaseneta mashuhuri kutoka chama cha demokrate wanaisihi serikali kutosubiri mpaka ufanyike uchaguzi wa bunge uliopangwa mnamo wiki mbili kabla haijatangaza mpango mpya juu ya Irak kwa ajili ya kudhaminia usalama wa nchi hiyo. Lakini hadi sasa, rais George W. Bush hayuko tayari kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake kutoka Irak. Bush amesema:

´´Mimi ni mtu mwenye subira. Subira yangu si ya milele na si yakupoteza muda. Lakini ninafahamu kiwango cha matatizo yanalolikabili jukumu letu pale. Ndio tunawaambia raia wa Marekani: hatutasimamisha na kukimbia.´´