1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwanajeshi wa Marekani akatiwa hukumu ya maisha jela kwa mauaji nchini Irak

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCru

Mahakama ya kijeshi nchini Marekani imemhukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela mwanajeshi kutoka Marekani aliyapatikana na hatia ya kumubaka kabla ya kumuuwa msichana wa kiiraki wa miaka 14 pamoja na familia yake. Mwanajeshi huyo kwa jina James Baker, alikuwa miongoni mwa wanajeshi watano wa kikosi cha 10 cha wanajeshi wa angani ambao walituhumiwa kuhusika na mauaji ya tarehe 12 Machi mwaka huu katika kijiji kimojawapo karibu na mji wa Mahmudiyah, kusini mwa mji mkuu Baghdad.

Baker amekiri kuhusika na makosa yote yaliokuwa yakimkabili ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, kupanga mauaji, kwenda kinyume cha sheria na kutotii amri ya viongozi wake wa kijeshi. Na amekubali kutoa ushahidi dhidi ya watuhumiwa wengine wa makosa hayo.