1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwito kuwa na msimamo mmoja kuhusu Iran

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FP

Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Robert Gates ametoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuwa na msimamo mmoja kuhusu mgogoro wa kinyuklia wa Iran.Amesema,Iran yapaswa kuwekewa vikwazo vikali zaidi vya kiuchumi,ili kuishinikiza kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia.Kwa upande mwingine,China imefuta mkutano uliopangwa kufanywa siku ya Jumatano,kati ya wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani,kujadili mgogoro wa nyuklia wa Iran.Mkutano huo umeahirishwa hadi juma lijalo.