1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mwito kwa Pakistan kutimiza ahadi za uchaguzi

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A9

Marekani ambayo tangu muda mrefu humtazama Rais wa Pakistan Pervez Musharraf kama mshirika wake muhimu imesema kuwa inasumbuliwa na hatua iliyochukuliwa na Musharraf kutangaza hali ya hatari.Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice alipozungumza ziarani mjini Istanbul,alimhimiza Musharraf kutimiza ahadi yake kufanya chaguzi huru za bunge mwanzoni mwa mwaka ujao.India pia imetoa mwito wa kurejeshwa haraka hali ya kawaida katika nchi jirani iliyo na nguvu za kinyuklia.Wakati huo huo,Uingereza imesema,ina wasiwasi mkubwa na imeitaka Pakistan iendelee na uchaguzi kama ilivyopangwa.