1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Ni mwaka wa nne tangu majeshi ya Marekani kuivamia Iraq.

20 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHG

Katika mwaka wa nne tangu pale majeshi ya Marekani kuivamia Iraq, rais wa Marekani George W. Bush kwa mara nyingine tena amekataa miito ya kuyaondoa majeshi ya nchi hiyo.

Katika hotuba kwa njia ya televisheni , Bush amewataka raia wa Marekani kutoa muda zaidi kwa msukumo mpya wa usalama mjini Baghdad na amewataka wabunge wa chama cha Democratic katika baraza la Congress kuacha upinzani wao dhidi ya vita kwa kuupinga muswada wa matumizi ya kijeshi.

Wito huo wa Bush uliingiliana na maoni mapya ya raia yanayoonyesha kuwa Wairaqi wanaendelea kuwa na shaka na wanaamini kuwa majeshi yanayoongozwa na Marekani yanahusika katika kuharibika kwa hali ya usalama nchini mwao.