1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Pendekezo la Bush lakataliwa bungeni

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnS

Rais George W.Bush wa Marekani amepata pigo kubwa bungeni katika pendekezo la kutaka kufanya mageuzi katika sheria ya uhamiaji.Kwa hivyo, siasa ya uhamiaji ya hivi sasa nchini Marekani, huenda ikawa,haitofanyiwa mageuzi makuu mpaka baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka ujao.Mswada uliopendekezwa na Bush,ungefungua njia ya kuwapatia hadhi ya halali,kiasi ya wahamiaji milioni 12 wanaoishi Marekani kinyume na sheria. Bush alishindwa kuzuia upinzani hata ndani ya chama chake cha Republikan.

Baadhi kubwa ya wanachama wa Republikan wanasema mswada huo ungezidisha uhamiaji wa haramu na kuwanufaisha wale waliovunja sheria.