1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Rais Bush ahutubia taifa

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYP
Waziri mkuu wa India Manmohan Singh
Waziri mkuu wa India Manmohan SinghPicha: AP

Rais George W. Bush wa Marekani amelihutubia taifa na bunge la Marekani huko wananchi wa Marekani wakiwa na mashaka juu ya mpango wake wa kuongeza wanajeshi nchini Iraq na huku kukiwa na bunge jipya linalodhibtiwa na chama cha Demokrat.

Katika hotuba hiyo amesema Wamarekani lazima wawe na nia ya kukabiliana na changamoto ngumu na maadui walioazimia kutimiza haja zao mbaya.Amesema ili kuwa na mustakbali wa matumaini na fursa wananchi wote inabidi wawe wanaweza kumudu huduma za afya na amependekeza kupunguzwa kwa kodi ya bima ya afya.

Pia katika hotuba yake hiyo Bush amesema atawasilisha bajeti ambayo itafutilia mbali nakisi ya serikali katika kipindi kisichozidi miaka mitano.

Maafisa wa Ikulu ya Marekani walisema Bush katika hotuba hiyo ataliomba bunge la Marekani kutoukataa mpango wake kwa Iraq. Mbali ya suala la afya hotuba yake hiyo inalenga suala la nishati ikiwa ni pamoja na lengo la kupunguza matumizi ya gesi ya Marekani kwa asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba theluthi mbili ya Wamarekani wanapinga uamuzi wa Bush wa hivi karibuni kutuma wanajeshi wa ziada 21,000 nchini Iraq wakati umwagaji damu ukizidi kupamba moto nchini humo.