1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Bush asaini sheria mpya dhidi ya serikali ya Hamas

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChI

Rais George W Bush wa Marekani amesaini sheria inayopiga marufuku kupekekewa misaada serikali ya Palestina inayoongozwa na chama cha Hamas mpaka itakapokubali haki ya Israel kuwepo na kukomesha ugaidi.

Sheria hiyo hata hivyo inaruhusu msaada upelekwe kwa rais Mahmoud Abbas, ambaye Marekani inamthamini kama mshirika wake. Kwa mujibu wa sheria hiyo maofisa wa chama cha Hamas hawatapewa visa za kusafiri kuingia Marekani, lakini inaruhusu Marekani ipeleke misaada ya kiutu kwa wapalestina.

Sheria hiyo inatenga kiasi cha dola milioni 20 kugharamia harakati za kuleta demokrasia na amani kati ya Israel na wapalestina.