1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Rais Bush asema halazimishwi na mtu kufanya maamuzi.

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjW

Rais wa Marekani George W. Bush amesema kuwa hatalazimishwa kufanya maamuzi ya haraka katika mpango wa mabadiliko ya sera kuelekea Iraq. Bush amekuwa akifanya mikutano mbali mbali na maafisa wa ngazi ya juu wa Iraq na Marekani, akikusanya mawazo na uzoefu kwa ajili ya uwezekano wa kubadili mikakati. Hii inakuja baada ya uamuzi wake wa kuchelewesha kutangaza mwelekeo mpya hadi mwakani, licha ya matarajio kuwa angefanya hivyo kabla ya Krismass.

Kumekuwa na ghasia zaidi nchini Iraq jana ikiwa watu 30 wameuwawa katika mashambulio kadha ya mabomu. Siku ya Jumanne, watu 70 wameuwawa na wengine 200 wengine wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mji mkuu Baghdad.