1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais George Bush akiri kaidhinisha kukabiliwa Wairan.

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXb

Rais wa Marekani, George W. Bush, amethibitisha taarifa iliyochapishwa na gazeti la Washington Post kwamba aliagiza vikosi vya Marekani vilivyoko Iraq kuwaua au kuwakamata raia wa Iran watakaotuhumiwa kuwa hatari kwa usalama.

Rais George Bush alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House baada ya kukutana na mkuu mpya wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, Luteni Jemedari David Petraeus.

Rais George Bush alitoa taarifa hiyo punde baada ya mkuu huyo mpya wa majeshi kuidhinishwa na baraza la Senate.