1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais wa Pakistan ahimizwa kuondosha hali ya hatari

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJm

Rais wa Marekani,George W.Bush amempongeza Rais wa Pakistan,Pervez Musharraf kwa hatua ya kutangaza kujiuzulu kwake jeshini na kuitisha uchaguzi mkuu.Lakini,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice akisifu uamuzi wa Musharraf amesema,hizo ni hatua muhimu zinazohitajiwa ili kuweza kuirejesha Pakistan katika njia ya kidemokrasia.Akaongezea kuwawanamhimiza pia kuiondosha hali ya hatari na lazima iondoshwe upesi iwezekanavyo.

Wakati huo huo,kiongozi wa upinzani nchini Pakistan,Benazir Bhutto amefurahia tangazo la Rais Musharraf kuitisha uchaguzi katika mwezi wa Januari.Lakini amesema,hiyo ni hatua ya kwanza tu.