1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rice aanza ziara yake ya Mashariki ya Kati

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6v

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, ameanza ziara yake ya Mashariki ya Kati. Hii leo anatarajiwa kuwasili Saudi Arabia ambako atafanya mazungumzo na mfalme Abdullah.

Baadaye atakwenda Misri ambako amepangiwa kukutana na rais Hosni Mubarak na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Ahmed Abu Gheit.

Bi Rice atazitembelea Israel na Palestina ambako atakutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Condoleezza Rice anataarajiwa pia kuitembelea Jordan.