1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Serikali ya Irak haikufanya maendeleo

5 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSW

Tume Huru ya Ukaguzi ya Marekani inasema,serikali ya Irak imeshindwa kuleta utulivu nchini.Ripoti hiyo inasema,serikali ya Waziri Mkuu wa Irak,Nuri al-Maliki katika miezi michache iliyopita imeshindwa kupatanisha makundi ya kikabila na ya madhehebu mbali mbali.

Vile vile,hakuna maendeleo yaliyopatikana kuhusu sheria ya kugawana kihaki pato la mafuta na pia haijulikani,vipi serikali ya Irak imetumia msaada wa kiuchumi wa Dola bilioni 10 uliotolewa na Marekani.Chama cha upinzani cha Wademokrats nchini Marekani kinasema,ripoti hiyo ni ushahidi kuwa mkakati wa Rais George W.Bush kuhusu Irak, haujafanikiwa.