1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Serikali ya Iran itashinikizwa zaidi

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBO2

Marekani na Ufaransa zinataka kuishinikiza zaidi serikali ya Iran kuhusu miradi yake ya nyuklia. Hata hivyo,Rais George W.Bush wa Marekani amesema,bado ana matumaini ya kuisadikisha Iran, kuachilia mbali mipango yake ya nyuklia kwa njia za kidiplomasia.

Rais Bush amesema,wataendelea kuishinikiza Iran.Juu ya hivyo,lengo ni kupata suluhisho la amani.

Hata Waziri wa Masuala ya Nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner ameimarisha msiamamo wake kuhusu mgogoro wa nyuklia.Alipozungumza mjini Washington, Kouchner alisema,Iran iliyo na silaha za nyuklia, ni wazo lisilokubalika.Leo Ijumaa,wajumbe wa nchi tano zenye kura turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, wanakutana mjini Washington,kushauriana juu ya uwezekano wa kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran.