1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Steinmeier aendelea na ziara yake ya Marekani

20 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHC

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujrumani, Frank Walter Steinmeier, anaendelea na ziara yake mjini Washington Marekani. Steinmeier amesema mpango wa ulinzi wa Marekani wa kuweka makombora mashariki mwa Ulaya hauharibu uhusiano baina ya Ulaya na Marekani.

Huku Ujerumani na Marekani zikijaribu kupunguza tofauti zao, waziri wa mashauiri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema mfumo huo wa ulinzi unatakiwa kuiimarisha Ulaya. Amesema Marekani inaendelea na mashauriano na washirika wake barani Ulaya na Urusi ambayo inaupinga mpango huo.

Waziri Steinmeier anaamini kwamba Marekani inafahamu mwito wa kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, kuwepo na mazungumzo juu ya swala hilo.