1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Syria kushiriki kenye mkutano wa amani ya mashariki ya kati

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBN2

Marekani imesema kwamba itazialika nchi kadhaa za kiarabu ikiwemo Syria katika mkutano wa amani ya Mashariki ya Kati utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu mjini Washington.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amesema hayo baada ya mkutano uliofanyika mjini New York uliozihusisha pande nne zinazoshughulikia mpango wa amani ya mashariki ya kati zikiwa ni Marekani,Uingereza, Umoja wa Ulaya na Urusi.

Kati ya nchi za Kiarabu zitakazo alikwa kwenye mkutano huo ni Misri na Jordan pekee ndizo zilizokwisha tia saini makubaliano ya amani na Israel.