1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Tume ya Marekani kutangaza sera mpya kuhusu Irak

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCo7

Tume maalum iliyoundwa na serikali ya Marekani kuchunguza sera za serikali hiyo kuhusu vita vya Irak,imekubali mapendekezo yaliotolewa na wajumbe wake.Tume hiyo yenye wajumbe kutoka vyama vya Republikan na Demokratik chini ya uongozi wa aliekuwa waziri wa mambo ya kigeni James Baker, itatoa ripoti yake Jumatano ijayo.Serikali ya Marekani inatumai kuwa mapendekezo ya sera mpya za Irak yatatoa njia mpya ya kujiondoa kwenye mgogoro wa Irak.Kwa mujibu wa ripoti za gazeti la „New York Times“ miongoni mwa mambo yalioshauriwa na wataalamu wa tume hiyo,ni kuondosha vikosi vya Marekani kwa awamu,kuanzia mwaka ujao.