1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wabunge wa Marekani waupinga mpango wa Bush

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbO

Wabunge wa Marekani wameukosoa mpango wa rais George Bush kutaka kupeleka wanajeshi 20,000 zaidi wa Marekani kwenda Irak. Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mahusiano ya kigeni wa chama cha Democratic, Joe Biden, ameuleza mpango wa rais Bush kuwa kosa kubwa.

Mbunge Joe Hagel wa chama cha Republican cha rais Bush, ameeleza pia msimamo kama huo.

´Nafikiri hotuba iliyotolewa na rais Bush inadhihirisha kosa kubwa na hatari kabisa la kisera nchini humu tangu vita vya Vietnam ikiwa mpango huo utatekelezwa. Nitaupinga.´

Viongozi hao wametoa matamshi yao wakati waziri wa mashauri ya kigeni wa Mardkani Condoleezza Rice alipoutetea mpango wa rais Bush mbele ya kamati hiyo ya bunge. Bi Rice alisema ni jukumu la serikali ya Irak, kuhakikisha mpango huo unafaulu.

Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates, ameiambia kamati inayoshughulikia maswala ya jeshi ikiwa serikali ya Irak haitatimiza majukumu yake huenda wanajeshi wa ziada wasitumwe kwenda Irak.