1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Wademocrats wapinga bado mpango wa rais kuhusu Iraq.

20 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8n

Rais wa Marekani George W. Bush na wanachama wenzake wa chama cha Republican wanaendelea na mjadala na baraza la Congress ambalo linadhibitiwa sasa na chama cha Democratic juu ya vita nchini Iraq.

Katika huenda matamshi ya kuleta matumaini hadi sasa, kiongozi wa baraza la Seneti wa chama cha Democratic Harry Reid, amesema kuwa Marekani itakuwa imeshindwa vita iwapo utaratibu wa kijeshi wa hivi sasa utafuatwa.

Warepublican wamesema baada ya matamshi hayo kuwa taarifa hiyo ni ushahidi kuwa Wademocrat hawaungi mkono majeshi huko Iraq.

Wakati huo huo katika ziara yake nchini Iraq waziri wa ulinzi Robert Gates amewaambia viongozi wa Iraq kuwa wanapaswa kuzidisha juhudi zao za kupata muafaka kati ya makundi ya kidini yanayopigana.

Ameongeza kuwa juhudi za Marekani nchini Iraq sio za milele.