1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wakala wa zamani aituhumu serikali ya Bush

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCI6

Baada ya kubakia kimya kwa muda wa miaka minne, wakala wa zamani wa shirika la upelelezi la Marekani-CIA-Bibi Valerie Plame,ameituhumu serikali ya Bush kuwa hapo mwaka 2003,kwa makusudi ilitoa siri yake kwa sababu za kisiasa. Alipozungumza mbele ya halmashauri ya Baraza la Wawakilishi la Marekani alisema,serikali ya Bush ilitaka kumuaibisha yeye na mumewe ambae hadharani alikosoa vita vya Irak.Kwa maoni yake, mshauri mkuu wa Bush,Karl Rove ndio aliyetoa siri hiyo kwa waandishi wa habari.Lakini mapema mwezi huu,Lewis “Scooter” Libby aliekuwa mshauri mkuu wa Makamu wa Rais Dick Cheney,alikutikana na hatia ya kuzuia uchunguzi kufanywa kuhusu kisa cha kutolewa siri ya Plame.Wakala huyo wa zamani amesema,kwa sababu ya vitendo vya aina hiyo vya kutoa siri,katika siku zijazo,wale wanaotaka kujiunga na CIA,watafikiria mara mbili.