1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wamarekani walichagua bunge jipya

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv7

Raia nchini Marekani wameanza kupiga kura kuwachagua wabunge. Watu milioni 200 ndiwo wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua wajumbe 435 wa baraza la wawakilishi na wajumbe 35 wa baraza la senet juu ya jumla 100 wanaounda baraza hilo.

Wademokrate wanatumai kupata ushindi kulidhibiti baraza mojawapo kama sio yote mawili.

Kampeni ya uchaguzi ilihusu hasa namna rais George W.Bush kutoka chama cha Republikan anavyoendesha vita nchini Irak.

Katika siku ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi jana, kila upande ulidai kuwa utashinda.

Kiongozi wa kampeni kwa ajili ya chama cha demokrate, Charles Schumer, alisema wao wanatumai kupata ushindi hata katika baraza la senet:

´´Kutakuwa na ushindani mkubwa. Tunakaribia kupata ushindi wa senet. Kwa sasa, hatuwezikufungua champain au kusherehekea, lakini tuko katika hali nzuri tu´´.

Rais Bush anaamini badala ya kumdhuru na chama chake cha republikan, siasa zake juu ya Irak zitamsaidia:

´´Hatua yangu ya kumtoa madarakani, Saddam Hussein, ilikuwa ni hatua nzuri na hali sasa ni bora duniani kutokana na hilo´´.