1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wanachama wa Mafia waliajiriwa kumuua Rais Castro

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBny

Shirika la upelelezi la Marekani-CIA,liliajiri wanachama wa Mafia,kujaribu kumuua Rais wa Cuba Fidel Castro.Hilo ni miongoni mwa yale yaliyofichuliwa na hati zilizowekwa bayana,kwenye tovuti ya CIA katika mtandao wa Internet.Hati hizo vile vile zinaeleza kwa umbali gani shirika hilo lilimpeleleza adui wake wa enzi ya Vita Baridi,Soviet Union ya zamani pamoja na hata waandishi wa habari na raia wa Kimarekani waliopinga vita vya Vietnam.