1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Watu tisa wafa Marekani kwenye ajali ya daraja.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcs

Watu kiasi tisa wamefariki dunia kutokana na ajali ya kuporomoka daraja linalovuka mto Mississippi mjini Minneapolis nchini Marekani.

Daraja hilo lililo kwenye barabara kuu limeporomoka wakati wa harakati nyingi ambapo magari kadhaa yalitumbukia mtoni.

Taarifa za awali zilisema magari kati ya hamsini na mia moja yalikuwa kwenye daraja hilo likiwemo basi la shule lililokuwa limebeba watoto sitini.

Watoto kumi walilazwa hospitalini.

Mkuu wa idara ya zima moto ya Minneapolis, Jack Clack, amesema watu kiasi sitini walijeruhiwa na huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.

Polisi wamesema sababu za ajali hiyo hazijajulikana, ingawa wamekanusha uwezekano wa ajali hiyo kuwa imesababishwa na vitendo vya kigaidi.