1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wito kuchunguza madai ya mateso

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCID

Wabunge wawili wa Marekani wanasema,madai ya mtuhumiwa mkuu wa Al Qaeda,Khalid Sheikh Mohammed kuwa aliteswa na shirika la upelelezi la Marekani CIA yanapswa kuchunguzwa.Maseneta Carl Levin na Lindsey Graham waliohudhuria kikao cha siri kuhusika na Mohammed,kwenye jela ya Guantanamo Bay wamesema,sifa ya Marekani itaathirika kama madai hayo hayotochunguzwa.Kwa mujibu wa nakala ya matamshi ya Mohammed,iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon mtuhumiwa huyo amedai kupanga au kutekeleza mashambulizi 30,ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001. Kikao cha kumsikiliza mtuhumiwa Khalid Sheikh Mohammed kilifanywa kwa siri siku ya Jumamosi katika kituo cha Guantanamo Bay.Hakuna waandishi wa habari waliozuiliwa kwenye kikao hicho cha siri.