1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wito kuiwekea Iran vikwazo zaidi

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNg

Madola makuu yamekutana mjini Washington kujadili uwezekano wa kuiwekea Iran vikwazo zaidi,baada ya nchi hiyo kukataa kutekeleza wito wa Umoja wa Mataifa kusita kurutubisha uranium.Wana diplomasia wa nchi tano zenye uanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani,wamekutana kujadili azimio jipya kwa azma ya kuishinikiza Iran.China na Urusi zinasita kuiwekea Iran vikwazo zaidi, zikisema kuwa hivi karibuni,Iran iliamua kushirikiana na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA.Nchi za magharibi zina hofu kuwa mradi wa Iran unaweza kutumiwa kutengeneza silaha za nyuklia.