1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Al Qaida aliyelipua hotel huko Mombasa, apelekwa Guantanamo Bay

27 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF2

Mtuhumiwa wa shambulizi la kigaidi katika Hoteli ya Kitalii nchini Kenya mwaka 2002, Abdul Maliki amepelekwa katika gereza la Guantanamo Bay, baada ya serikali ya Kenya kumkabidhi kwa Marekani.

Abdul Maliki anatuhumiwa kuwa gaidi wa kundi la Al Qaida, na kuhusika na shambulizi la kigaidi katika hoteli ya Paradise inayomilikiwa na raia wa Israel Mombasa nchini Kenya, ambapo watu 13 waliuawa.

Msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon, Bryan Whiteman amesema kuwa mtuhumiwa huyo ni gaidi hatari, na kwamba amekiri kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo msemaji huyo wa Pentagon, hakutaja uraia wa mtuhumiwa huyo.