1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Baridi kali yaleta madhara

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaI

Siku nne za baridi kali, katika majira ya baridi, theluji na upepo mkali katika eneo la magharibi kati nchini Marekani zimesababisha watu zaidi ya 30 kupoteza maisha.

Eneo lililoathirika zaidi ni majimbo ya Missouri na Oklahoma, ambako mamia kwa maelfu ya watu wameachwa bila ya umeme kutokana na upepo mkali na hali ya baridi.

Upepo huo mkali ulianza siku ya Ijumaa kutokana na upepo mkali kutoka katika eneo la Arctic ambao ulivuma kupita katikati ya Marekani kutoka Canada hadi Texas. Hata jimbo la Califonia liliathirika na hali ya baridi kali, ambako mazao kadha wameharibiwa.