1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON;Bush aidhinisha mpango wa kuweka kituo cha majeshi ya Marekani barani Afrika

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUN

Rais G . Bush ameidhinisha mpango wa nchi yake juu ya kuweka kituo maalumu cha majeshi ya Marekani barani Afrika.Marekani imesema kituo hicho kitasaidia katika kutekeleza maslahi ya kijeshi ya Marekani na hasa katika harakati za kupambana na ugaidi.