1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON.Bush asema Marekani itaendelea kubakia Irak

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0B

Rais George W Bush wa Marekani amefanya mazungumzo kwa njia ya video na makamanda wake wa kijeshi juu ya hali ya Irak.

Takriban wanajeshi 80 wa Marekani wameuwawa katika mwezi huu wa oktoba pekee nchini Irak, hii ni idadi kubwa kuwahi kutokea tangu majeshi hayo yalipovamia Irak mwaka 2003.

Pamoja na hayo rais Bush amesisitiza katika hotuba yake ya radio ya kila juma kuwa hali hiyo haitabadilisha azma na lengo la Marekani nchini Irak.

Kituo cha Televisheni cha kiarabu cha Al Jaazera kimemnukulu afisa wa cheo cha juu katika jeshi la Marekani akisema kwamba nchi yake imeonyesha kutokujali na upumbavu wa hali ya juu nchini Irak.

Ikulu ya White House imekanusha kauli hiyo na msemaji wa ikulu amesema kuwa kauli ya afisa Alberto Fernandez imetangazwa kinyume na alivyosema.