1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush ataka bilioni 200 kwa ajili ya vita

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DV

Rais George Bush ametoa ombi la dola bilioni 200 kwa ajili ya kugharimia shughuli za kivita mwaka ujao.

Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vita za nchini Irak na Afghanistan.Ikiwa bunge la Marekani litakubali ombi hilo, gharama za vita zitavuka kiasi cha dola bilioni 750 tokea utawala wa rais Bush uzindue kampeni ya kupambana na ugaidi baada ya magaidi kuishambulia Marekani tarehe 11 mwezi septemba miaka sita iliyopita.