1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:China , Marekani katika mazungumzo ya kiuchumi

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzO

Ujumbe wa ngazi ya juu wa China ukiongozwa na Makamu wa Waziri Mkuu Wu Yi uko nchini Marekani kwa mazungumzo ya mapatano ya kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Ajenda kuu katika mazungumzo hayo itakuwa biashara na thamani ya sarafu ya China.

Kabla ya mkutano huo wa kwanza, Waziri wa fedha wa Marekani Henry Paulson alisema mtazamo ni juu ya soko la China.

Marekani pia inatarajiwa kuzungumzia kasi ya ukuaji wa uchumi wa China iliyofanyiwa mabadiliko.